Faini mwendokasi yang’ata magari 80
ZAIDI ya magari 80 yalikamatwa na madereva kutozwa faini mwishoni mwa wiki kwa kosa la kushindwa kufuata ukomo wa mwendokasi (overspeed), wakisafiri kupitia barabara ya Morogoro mkoani Pwani.
Zoezi la kukamatwa kwa magari hayo lilikuwa likiendeshwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Pwani wakishirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na kamati ya usalama ya barabara mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa sheria ya barabara ya mwaka 2007, Tanroads ina mamlaka ya kutoa adhabu kwa dereva atakayekutwa na makosa mbalimbali ya barabarani, likiwamo kuzidisha mwendo.
Sheria hiyo inaelekeza adhabu ya kutozwa faini ya Sh. 200,000 papo hapo ama kifungo cha miaka mitatu jela ama vyote viwili.
Akizungumza baada ya kumaliza zoezi hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani mkoani Pwani, Josephine Protace, alisema zoezi hilo ni endelevu na wanaendelea kutoa elimu kwa madereva wote, ili kufuata sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali, kwani idadi kubwa ya ajali zote zinazotokea husababishwa na mwendokasi.
“Wenzetu wa Tanroads wametushirikisha katika zoezi hili, ambalo ni endelevu, tumeanza na mwendokasi, lengo ni kuhakikisha tunawabaini madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kuwatoza faini, ili liwe fundisho kwa madereva wengine wenye tabia kama hiyo,” alisema Protace.
Alifafanua sheria hiyo siyo mpya bali ilikuwapo, hivyo Tanroads wanaitekeleza.
“Tukiwa katika hii operesheni baadhi ya madereva waliotozwa faini walilalamika kuwa faini ni kubwa, lakini faini hiyo ni kwa mujibu wa sheria, kwa hiyo natoa wito wafuate sheria za usalama barabarani, ili waepuke ajali, lakini pia waepuke faini ambazo wanadai ni kubwa,” Protace.
Ofisa leseni wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Pwani, Wilson Kalemera, alisema wanashirikiana na Tanroads katika zoezi hilo na wamekuwa wakikagua stika za mamlaka hiyo na kwamba wafanyabiashara wasiokuwa na stika zake watatozwa faini ya Sh. 250,000.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kibaha, Innocent Feksi, aliwataka madereva kutii sheria za usalama barabarani, ili kumaliza ajali sambamba na kuepuka faini wanazoweza kutozwa wanapokutwa na makosa ya barabarani.
USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA MBINDA BLOG IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI, nenda play store kisha tafuta / search MBINDA BLOG

Post a Comment