FULL VIDEO: Ripoti ya MCT kuhusu Makonda kuvamia wa Clouds Media Group

Leo Agosti 14 2017 Baraza la Habari Tanzania chini ya katibu wake mtendaji Kajubi Mkujanga imezunduliwa ripoti ya tukio la uvamizi wa kituo cha Clouds Media Group.

Ripoti hiyo iliyosomwa na Mwanasheria mwandamizi Juma Thomas ambaye ni Mwenyekiti wa kamati iliyokuwa na watu wanne, imesema Kitendo cha Makonda kwenda kwenye kituo cha Clouds Media ni kukiuka na kinyume cha Huduma za vyombo vya habari ambapo ripoti hiyo imeweka wazi kuwa Makonda aliingilia uhuru wa Vyombo vya habari na Uhariri wa Habari.

Ripoti hiyo inasema Makonda alitafutwa na timu ya uchunguzi bila mafanikio, na hata walipomwandikia barua hakuna chochote alichojibu, kwahiyo alijiondolea mwenyewe haki ya kusikilizwa.

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI



USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA MBINDA BLOG IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI, nenda play store kisha tafuta / search MBINDA BLOG

No comments