MZIMU WA WEMBLEY WAZIDI KUWAANDAMA TOTTENHAM
Manchester City wamepanda kileleni mwa ligi kuu ya Epl baada ya kuichapa bila huruma Watford mabao 6 kwa 0, huku Sergio Aguero akipiga hattrick na mengine yakifungwa na Raheem Sterling, Gabriel Jesus na David Silva.
Mabao ya leo yanamfanya Kun kufikisha junla ya mabao 200 ya soka lake barani Ulaya huku mabao 74 akiwafungia Atletico Madrid na 126 akiwafungia Manchester City.
Liverpool walipiga mashuti mengi zaidi msimu huu langoni mwa Burnley(mashuti 35) lakini wakapata suluhu ya bao 1 kwa 1 na Burnley huku bao la Liva likifungwa na Mohamed Salah huku lile la Burnley likifungwa na Scott Arfield.
Tottenham nao kwa mara ya kwanza wameshindwa kufunga bao katika uwanja wa nyumbani tangu January 2016 na hii ikiwa mara yao ya kwanza tangu 2013 kucheza michezo mitatu nyumbani bila ushindi baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na City.
Katika michezo mingine ya Epl Leicester City walitoka suluhu na Huddersfirld Town, Roy Hodgson akaanza na mkosi baada ya Crystal Palace kupigwa bao 1 kwa nunge na Southampton huku Newcastle United wakiipiga 2 kwa 1 Stoke City.
Kule Hispania wakati Levante wakienda suluhu na Valencia ya bao moja kwa moja, Barcelona walitoka nyuma ya bao moja la kutangulia la Getafe baada ya Dennis Suarez kusawazisha na Paulinho kuongeza bao la pili na kuufanya mchezo kuisha kwa bao 2 kwa 1.
Post a Comment