VIJANA ZAIDI YA 200 WA KITANZANIA WANUFAIKA NA MPANGO WA ELIMU WA MAREKANI

Zaidi ya vijana mia mbili kutoka baadhi ya shule za msingi na sekondari za serikali hapa nchini wamenufaika na mpango wa elimu wa unaoendeshwa na serikali ya Marekani ambao hutolewa kwa awamu tofauti za miaka miwili miwili.

Program hiyo iliyoanzishwa mwaka 2004 tayari imenufaisha zaidi ya vijana laki moja kutoka mataifa mbalimbali duniani, inalenga kukuza uelewa wa vijana hasa wa Afrika kwenye medani ya Lugha na matumizi yake katika kujijengea uwezo wa kukabiliana na mazingira yoyote ndani ya jamii.

Hapa nchini, kwa mwaka huu pekee jumla ya vijana mia mbili wamefanikiwa kumaliza kozi ya lugha ya kiingereza na matumizi yake iliyojumuisha mafunzo kwa vitendo, yaliyoambatana na ziara katika jamii zenye kuzungumza lugha hiyo.

Brinille Ellis ni mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, wakati wa kuwapongeza vijana 25 waliomaliza mafunzo katika kituo cha JOMAK cha Dar es Salaam, ameeleza vigezo vinavyotumika kupata wadau katika mpango huo.

Baadhi ya wazazi waliohudhuria hafla hiyo, wametoa ushahidi wa mafanikio yaliyofikiwa na vijana kwenye jamii kutokana na mafunzo waliyopata chini ya ubalozi wa Marekani hapa nchini .



No comments