ZITTO KABWE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA NYUMBA YAKE KUUNGUA MOTO LEO


Zitto Kabwe


Tumepata ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia.


Nawashukuru Jeshi la Zimamoto, majirani zangu pamoja na wananchi wenzangu kwa ushirikiano walioutoa mpaka kuuzima moto husika. Kwa sasa Jeshi la Polisi wanafanyia kazi kujua chanzo cha ajali.


Naomba wananchi wewe watulivu wakati Polisi wanaendelea na uchunguzi husika.


Nairobi - Kenya
Septemba 16, 2017



No comments