"kuna watu wanataka kumpindua Trump" Ikulu imesema

Afisa wa mawasiliano wa muda mfupi katika ikulu ya Marekani, Anthony Scaramucci, amesema kuna watu ndani ya serikali, ambao wanataka kumtoa madarakani Rais Trump.

Akizungumza na televisheni ya ABC, alisema Bwana Trump analengwa, kwa sababu hakuwamo kati ya viongozi wa siasa nchini humo.
Alipoombwa ataje majina, Bwana Scaramucci alisema, ameshawataja, na rais anahitaji kuleta watu zaidi walio watiifu kwake.

Alipohudumu kwa siku kumi, Bwana Scaramucci alikosoa watu kadha, pamoja na mkuu wa ofisi ya rais wa zamani, Reince Priebus.

Anthony Scaramucci (katikati) alifutwa baada ya kanda ya sauti kufuja akimtukana mshauri Steve Bannon (kushoto) na Reince Priebus


USISAHAU KUPAKUA / KUDOWNLOAD APPLICATION YA MBINDA BLOG IPO PLAY STORE ILI UPATE HABARI KWA URAHISI, nenda play store kisha tafuta / search MBINDA BLOG

No comments