UINGEREZA YAFANYA MSAKO MKALI WA MAGAIDI LONDON, NI KUFUATIA SHAMBULIO KATIKA STESHENI YA TRENI CHINI YA ARDHI
Serikali ya Uingereza inawasaka washukiwa wa shambulizi lililotokea katika stesheni ya treni ya chini ya ardhi, ambalo limesababisha kujeruhiwa kwa zaidi ya watu 20 katika kipindi hiki ambacho mamia ya wanajeshi wametawanywa katika maeneo tofauti ya taifa hilo.
Jana jioni serikali ilipandisha kiwango cha kitisho cha ugaidi na kuwa cha juu, baada ya bomu kuripuka katika muda wa pirikapirika nyingi, ikiwa na maana kuwa vyombo vya usalama vina imani ya kutokea shambulizi jingine hivi karibuni.
Wanajeshi wataongeza nguvu katika maeneo ya wazi ambayo polisi wameshika doria leo hii kwa lengo la kudhibiti shambulizi lolote.
Hadi wakati huu hakuna yeyote aliyetiwa mbaroni kufuatia shambilizi hilo.
Post a Comment