1930 ARSENAL WALIIADHIRI CHELSEA, 2014 WAKAADHIRIKA WAO,LEO NANI KUIBUKA KIDEDEA?
October 29 mwaka 2011 kama unakumbuka ndio ilikuwa mara ya mwisho ambapo Arsenal waliitembelea Chelsea na kupata ushindi, Arsenal waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 5 kwa 3.
Lakini kati ya kitu ambacho hukifahamu ni kwamba toka vilabu hivi vianzishwe Arsenal wamekuwa wakiifunga Chelsea Stamford Bridge mara nyingi, michezo 89 waliyokutana Stamford Bridge Arsenal wameshinda mara 39 huku Chelsea akishinda mara 24.
Lakini katika michezo 10 iliyopita kati ya Chelsea na Arsenal zilizopigwa katika uwanja huu Arsenal wamepata ushindi mara mbili wakipigwa mara nane huku kipigo kikubwa zaidi ikiwa kile cha tarehe 22 March 2014 wakati Arsenal wakifa bao 6 kwa 0.
Michezo miwili iliyopita katika msimu uliopita wa Epl hakukuwa na mbabe kwani Arsena waliibamiza Chelsea bao 3 kwa 0 katika uwanja wao wa Emirates lakini Chelsea wakawasubiri Arsenal Stamford wakawapiga bao 3 kwa 1.
Kipigo kikubwa Arsenal kuwachapa Chelsea ilikuwa tarehe 28 November mwaka 1930 ambacho Gunners waliichapa Chelsea bao 5 kwa 1 lakini kipigo kikubwa kabisa Chelsea kuwapa Arsenal ilikuwa kile cha mwaka 2014 cha mabao 6 kwa nunge.
Chelsea ambao wanatoka kuidhibu Fc Quarabag bao 6 kwa 0 watakuwa kwenye moto wa kuiteketeza Arsenal huku Alvaro Morata anayeonekana kuzidi kuimarika ataongoza safu ya mashambulizi kwa Chelsea hii leo.
Arsenal nao ambao wametoka kuipiga Koln bao 3 kwa 1 kati kati ya wiki watakuwa na mshambuliaji wao Alexis Sanchez ambaye inaeleweka ni hatari linapokuja suala la kuwaumiza wapinzani.
Chelsea wanaweza wakapewa nafasi kubwa katika mchezo huu wa leo kutokana na rekodi za nyumbani dhidi ya Gunners lakini Arsenal sio wa kuchukulia poa hata kidogo na mchezo wa leo utakuwa kati ya michezo migumu kwa pande zote.
Post a Comment