MBUNGE WA CCM ALIYEKWENDA KUMTEMBELEA TUNDU LISSU AELEZA HALI YA LISSU ALIYOMKUTA NAYO
Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amemtembelea Hospitali alikolazwa Mbunge na Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi Dodoma ambapo baada ya kufika, ametueleza hali ya Tundu Lissu pamoja na anachohitaji Watanzania wafanye.
Japo hakuwa na uhakika kama Madaktari wangeruhusu kwenda kumsalimu Tundu Lissu, ruhusa ilitoka baadae ambapo baada ya kumuona na kuagana nae, Nyalandu amesema yafuatayo
“ukweli ni kwamba ameumizwa vibaya, Imeelezwa Madaktari wanaendelea na hatua kadhaa za matibabu, wakiwa wameanza kwa kumuimarisha ili kuufanya mwili uweze kumudu hatua zaidi za utibabu anazopaswa kufanyiwa“
Mengine yote aliyoyasema Nyalandu unaweza kuyafahamu kwa kubonyeza play hapa chini….
MSIKILIZE HAPA:
Post a Comment