UNICEF INAFANYA KAMPENI YA KURUDISHA WATOTO 150,000 WENYE UMRI WA KUSOMA SHULENI DRC.
UNICEF inafanya kampeni ya kurudisha watoto 150,000 wenye umri wa kusoma shuleni DRC.
Kampeni hiyo imefuatia mapigano kati ya wapiganaji na maafisa usalama yaliyosababisha maelfu ya familia kuyahama makazi yao.
Ripoti ziilizotolewa na UNICEF zinaonyesha kuwa watoto 850,000 hawapati haki zao za msingi kama elimu na huduma za afya toka kuanze kwa mapigano hayo.
Kwa mujibu wa habari,kampeni hiyo pia ina lengo la kutoa mafunzo kwa waalimu 2750.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa walimu na wauguzi wengi hasa Kasai wameuawa na wengine kuyakimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Post a Comment